ABOUT US

Victoria Foundation Ltd, ni Taasisi binafsi inayojishunghulisha na kusaidia watoto yatima na wasiojiweza wa mkoa wa Geita ambayo ilisajiliwa Januari 2011, kwa namba 81136. Makao Makuu ya Taasisi hii yako mkoani Geita .

Kutokana tatizo la kuwa na watoto wengi yatima, Taasisi hii iliona ni vema kuanzisha kitu kama hiki ili kuwasaidia katika mambo mbalimbali yakiwepo ada za shule, chakula na kuwaandalia muelekeo mzuri wa maisha yao ya baadae.

Victoria Foundation Ltd ina ardhi ya heka 40 katika eneo la Bombambili Geita mjini kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi unaotarajia kuanza hivi karibuni pia inasomesha wanafunzi 20 katika shule za Kata mkoani Geita.

Wakati huo huo Victoria Foundation Ltd pia ina ofisi ndogo eneo la Kijitonyama jijini Dar es Salaam.